WARSHA YA UTAMADUNI, KITUO CHA UTAMADUNI (MAKUMBUSHO YA WASUKUMA) BUJORA, TAREHE 11-23 JANUARI 2016.
Je, unapenda kujiunga nasi katika warsha ya Utamaduni Bujora?
Sasa unayo nafasi ya pekee kwa ajiri ya kushiriki, kujifunza na kufurahia tunu za utamaduni wa msukuma. Kituo cha Utamaduni (makumbusho ya wasukuma) Bujora wamekuandalia warsha kwa kila anayependa urithi wa utamaduni. Warsha hii inahusu mambo yafuatayo:
• Mafunzo ya kucheza, kuimba na kupiga ngoma pamoja na kikundi cha wasesilia Bujora
• Kutembelea vikundi mbalimbali vya ngoma vijijini, ikiwa ni pamoja na kujifunza pamoja nao
• Siku moja ya mashindano ya nyimbo toka kwa wamanju wote maarufu usukumani
• Siku moja ya mashindano ya ngoma kutoka vikundi walioshiriki na wengineo maarufu usukumani.
Zaidi ya hayo, utapata nafasi ya kutembelea mabanda ya makumbusho ili kuona jinsi utamaduni wa msukuma ulivyohifadhiwa. Kutakuwepo pia na chakula cha asili, na mfunzo ya kutengeneza Ngoma ( kuwamba Ngoma). Pamoja na kujifunza Lugha ya kiswahili na kisukuma.
RATIBA YA WARSHA
Siku ya Kwanza: Makaribisho uwanja wa ndege Mwanza, (Stendi ya Mabasi Mwanza) hadi Bujora
Siku ya Pili: Mafunzo ya Lugha ya kiswahili na kisukuma ( kwa wasiofahamu lugha hizo), kutembelea Makumbusho, na jioni kutakuwa na tafrija ya makaribisho ya wageni
Siku ya tatu: Kutakuwa na warsha ya ngoma na nyimbo kwa washiriki wote pamoja na wacesilia wa Bujora
Siku ya Nne, ya Tano na ya Sita : Kutembelea vikundi vijijini, warsha ya ngoma na nyimbo pamoja na vikundi huko vijijini.
Siku ya Saba : Mapumziko
Siku ya Nane : Warsha pamoja na kikundi cha wanacesilia Bujora
Siku ya Tisa na ya Kumi : Kutembelea vijijini, kufanya Warsha pamoja na vikundi huko.
Siku ya Kumi na Moja : Mashindano ya Nyimbo kutoka kwa wamanju maarufu usukumani (yatafanyika Bujora)
Siku ya Kumi na Mbili : Mashindano ya ngoma kwa vikundi vilivyoshiriki na vinginevyo maarufu usukumani. Zaidi ya vikundi kumi vitashiriki.
Siku ya Kumi na Tatu: Itakuwa siku ya kuagana na wageni wote na watasindikizwa mpaka uwanja wa ndege au stendi ya mabasi Mwanza.
GHARAMA
UMRI (MIAKA) NA KIASI
Miaka 18 na kuendelea: 4.000,- DKK (Denish korona)
Miaka 14 – 17: 2.500,- DKK
Miaka 7 – 13: 1.500,- DKK
Miaka 3 – 6: 500,- DKK
Miaka 0 – 3: BURE!
• Gharama hizi zinajumuisha Chakula, Malazi, Mafunzo na Usafiri kwa safari zote zitakazofanyika
• Kutakuwa na kikao kwa wote watakaopenda na watakaoshiriki warsha hiyo tarehe 03 Octoba 2015. Tafadhari jisajili kupitia baruapepe (Anuani) ifuatayo kwa ajili ya kushiriki kikao cha maandalizi, kuuliza maswali na kupata ushauri : warsha2016@sukumamuseum.org
NOTE: Wahi sasa ujisajili, nafasi ni yako