Kumbukumbu ya miaka 42 ya Daraja la Utamaduni

MWALIKO KUHUDHURIA MAONYESHO YA UTAMADUNI WA MSUKUMA YATAKAYOFANYIKA KATIKA MAKUMBUSHO YA MOESGÅRD HUKO ÅRHUS, DENMARK TAREHE 22-23 AGOSTI 2015.

Mpendwa wanautamaduni, kwa upendo mkubwa unaombwa kuhudhuria maonyesho tajwa hapo juu.

Tunakumbuka tangu mwaka 1973, kikundi cha ngoma cha WanaCesilia kutoka Makumbusho ya wasukuma Bujora, kwa mara ya kwanza kilifika katika Makumbusho ya Moesgård, na kucheza ngoma za kisukuma. Pia kiliweza kufanya maonyesho ya Ngoma katika nchi za Sweden na Norway mwaka huo.

Watu wengi walifurahia sana, na tokea hapo wadenish wengi walifika kutembelea makumbusho ya wasukuma Bujora na hatimaye kujenga mahusiano mazuri kati ya Wasukuma na Wadenish, mahusiano yaliyozaa DARAJA LA UTMADUNI (Cultural Bridge). Sasa imetimia miaka 42 tangu mahusiano haya yalipoanza.

Wewe ukiwa Msukuma na mpenda Utamaduni unayeishi hapa Ulaya ( hasa walioko Denimark) tunakualika rasmi ufike kushiriki nasi, pamoja na marafiki zako wote . katika maonyesho hayo kutakuwepo na michezo ya ngoma mbalimbali za kisukuma kama vile, Lugaya, Bunungule, Bugunda Sogota, Pachanga, Bugobogobo n.k. Katika Maonyesho hayo, tutapata pia nafasi ya kutembelea na kuona Makumbusho ya Moesgård.

Maonyesho hayo yatadumu kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 22-23 Agosti 2015, na yatakuwa yanaanza saa 4:00 Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni. Siku ya tarehe 23 kutakuwa na tukio maalum la mitambiko katika nyumba za MASAMVA ili kuwakumbuka wote waliofariki dunia, hasa wale waanzilishi wa DARAJA LA UTAMADUNI.

Unaombwa ufike siku ya Ijumaa ya tarehe 21 Agosti, saa 10 Jioni ÅRHUS, Nyumbani kwa SHOMA kwa anuani hii: GAMMEL SILKEBORGVEJ 9, 8462 HARLEV J

NOTE: TUNAOMBA SANA UFIKE BILA KUKOSA. FIKA NA TENTI KWA AJILI YA   KULALA